Isaiah 51:9-10


9 aAmka, Amka! Jivike nguvu,
ewe mkono wa Bwana,
Amka, kama siku zilizopita,
kama vile vizazi vya zamani.
Si ni wewe uliyemkata Rahabu vipande vipande,
uliyemchoma yule joka?

10 bSi ni wewe uliyekausha bahari,
maji ya kilindi kikuu,
uliyefanya barabara katika vilindi vya bahari
ili waliokombolewa wapate kuvuka?
Copyright information for SwhKC